PUBLIC NOTICE (TANGAZO KWA UMMA)

Prerequisites to access the BRELA online system (ORS)

(i) National Identification Number (NIN) from NIDA is required for all registrations service at BRELA

  • Only Tanzanian users who have National Identification Number (NIN) issued by the National Identification Authority (NIDA) will be able to access ORS services.
  • All Directors, Company Secretaries and shareholders of companies will have to provide their NINs in the ORS.
  • A local natural person will not be registered as a shareholder, director or Company Secretary without having a National Identification Number.

(ii) Foreigners who want to register a company

  • Must use particulars of their Passports issued by their respective Countries or National Identification Number (NIN) issued by the National Identification Authority (NIDA).

(iii) Tax Identification Number (TIN) issued by their Tanzania Revenue Authority (TRA)

  • A person will not be registered as a director without having a Tax Identification Number (TIN) for Tanzanians and Passport details for Foreigners

(iv) Preparation of Memorandum and Article of Association
The objectives in the Memorandum and Articles of Association to be uploaded to the ORS must be in line with the objectives to be selected through the ORS from the per ISIC Rev.4 Classification.
Click here to view ISIC Rev.4 Classification

Thus, to avoid frustrations BRELA management advises all persons currently having a role or intending to take a role of a company directors, shareholder, secretary or owner of business name, to immediately visit NIDA officers and obtain a National ID (if she/he does not possess one yet).

All current and future directors and shareholders, please, ensure that you have Tax Identification Number (TIN) from the TRA.

Mahitaji ya lazima za kuingia kwenye mfumo wa ORS ni kama yafuatayo;-
(i) Kuwa na namba ya Utambulisho wa Utaifa inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA)

  • Namba ya Utambulisho wa Utaifa ndiyo kitambulisho pekee cha kuingia kwenye mfumo wa ORS.
  • Wakurugenzi wa Kampuni, katibu wa kampuni pamoja na wanahisa wanatakiwa kuwa na Namba ya Utambulisho wa Utaifa na kama siyo watanzania wanapaswa kuwa na namba ya pasi ya kusafiria.
  • Kama ni mgeni (siyo Mtanzania) ambaye anatarajia kusajili Kampuni Tanzania anatakiwa awe na namba ya pasi ya kusafiria (Passport Number) au namba ya kitambulisho cha mgeni mkazi kinachotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
(ii) Wakati unaandaa Malengo na Katiba ya Kampuni (Memorandum and Article of Association) hakikisha malengo unayojiwekea yameendana na shughuli unazozichagua kwenye mfumo wa ORS kwa mujibu wa ‘ISIC classification’ ambayo inapatikana kwenye mtandao na kwenye Tovuti ya BRELA www.brela.go.tz

Ili kuepuka usumbufu na kuchelewa hakikisha unakuwa na namba ya utambulisho wa Utaifa pamoja na namba ya utambulisho wa mlipa kodi kabla ya kuanza taratibu za usajili. Kwa kampuni zilizosajili zilizowasilisha maombi ya kusajiliwa kabla ya tarehe 1 Februari 2018, tafadhali zingatia yafuatayo:-
(i) Kuwa na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (National Identification Number (NIN) inayotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA).
(ii) Wakurugenzi na Katibu wa kampuni kuwa na Namba ya Utambulisho wa mlipa kodi (TIN) na Namba ya Utambulisho wa Utaifa (NIN), kwa wasio Watanzania wawe na namba ya pasi ya kusafiria.
(iii) Ingia kwenye mfumo na uchague ‘Filing Annual Returns/Accounts ingiza taarifa muhimu.
(iv) Kuhakiki taarifa za kampuni yako katika ofisi ya Msajili wa Makampuni ikiwa nyaraka kwenye jalada lako hazijasajiliwa au hujawasilisha Mizania (annual returns) ya miaka ya nyuma.
Note:Bila kuweka nyaraka zako kwenye mfumo, hutaweza kuwasilisha taarifa/mizania ya Mwaka, kubadilisha Makatibu wa kampuni, taarifa za benki na kadhalika.