Online Registration System(ORS)The Business Registrations and Licensing Agency (BRELA) has completed the development of a modern Online Registration System (ORS), the system comprises registration of Companies, Business Names, Trade and Service Marks and their respective post registrations, issuance of Patents and Industrial Licenses. The system will enable customers to access all BRELA services wherever they are without visiting BRELA premises, at any time of the day. BRELA has started rendering services online in modules starting with Industrial Property services: Trade and Service Marks and Patents and Companies registrations.


In addition, the number of the registered company through ORS corresponds to the Registered Company's TIN ID Number. Therefore, you are advised to submit a company registration certificate to the nearest Tanzania Revenue Authority (TRA) office to collect the Company's TIN certificate.

Mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao (ORS)

Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imekamilisha kutengeneza mfumo mpana wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS) mfumo huu utatatoa huduma zote kwa njia ya Mtandao ikiwemo Usajili wa Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma pamoja na huduma zote baada ya usajili kwa njia ya Mtandao, aidha, Mfumo pia utatumika kwa utoaji wa Hataza na Leseni za Biashara.

Mfumo utawezesha watumiaji kupata huduma popote walipo wakati wowote bila kulazimika kufuata huduma hizo katika ofisi za BRELA.

Aidha, namba ya kampuni inayosajiliwa na BRELA kupitia mfumo wa ORS inawiana na Namba ya utambulisho wa Mlipa kodi (TIN) ya Kampuni iliyosajiliwa. Hivyo, unashauriwa kuwasilisha cheti cha usajili wa kampuni kwenye ofisi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyo karibu nawe uweze kuapta cheti cha TIN cha Kampuni yako.

BRELA imeanza kutumia mfumo huu kwa awamu ambapo tarehe 4 Januari 2018 ilianza kutoa hudum za Miliki Ubunifu kwa njia ya Mtandao kama vile kusajili Alama za Biashara na Huduma pamoja na Hataza.