Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

Kwanza utaunda akaunti mpya ya mtumiaji na kuhuisha, kisha andika barua kwa BRELA kutoa idhini ya kufikia akaunti hiyo na kisha kuhuisha taarifa katika mfumo wa ORS.

Unapaswa kusahihisha taarifa za TIN kupitia TRA ili zilingane na taarifa za NIDA.

Ndio, unaweza kutumia kitambulisho hicho cha Taifa lakini anwani tofauti ya barua pepe kuunda akaunti nyingi za ORS.

Unahitaji kuhuisha akaunti yako ya ORS ambayo ilihamishwa kutoka OBRS kwa kwenda kwenye kiunga cha wasifu kisha ingiza kitambulisho chako cha Taifa, bonyeza ingiza taarifa kutoka NIDA na kisha bonyeza vitufe vya kutunza/kuwasilisha.

Hapana, Majina yote ya Biashara yaliyosajiliwa katika OBRS yamehamishwa kwenye ORS na kuhuishwa kiautomatiki na mfumo wa ORS na kwa hivyo unaweza kuomba huduma zingine lakini sio kuhuisha taarifa za Majina ya Biashara yaliyomo.

Hupaswi kuunda akaunti mpya ya ORS kwani akaunti yako ya OBRS uliyotumia kusajili jina la biashara yako imehamishiwa ORS na kwa hivyo umetumiwa ujumbe katika anwani yako ya barua pepe uliyotumia wakati wa usajili pia katika ujumbe kuna jina la mtumiaji na nywila ya muda ambayo unaweza kutumia kuingia kwenye mfumo mpya wa ORS.

Mwombaji wa kwanza anayeomba huduma hiyo lazima amalize ombi la kwanza kabla ya kuanza ombi lengine.

Unatakiwa uripoti hii kwa BRELA kwa kutoa ombi au nambari ya kupigia mfano, G180101-0101.