Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Huduma Zetu

UTOAJI WA LESENI ZA BIASHARA KUNDI A

Leseni za biashara ni nini?

Ni kibali au ruhusa anayopewa mtu kwa ajili ya kumruhusu kufanya biashara.

Aina za Leseni

1. Leseni ya biashara kundi “A” hii hutolewa kwa biashara yenye sura ya kitaifa au kimataifa au inayoongozwa na sera.

2. Leseni ya biashara kundi “B” hii hutolewa kwa biashara ambayo haina sura ya kitaifa au kimataifa au isiyoongozwa na sera. Zinatolewa na Mamlaka za Serikali za Mitaa (Halmashauri/Manispaa).

Faida za kuwa na leseni ni zipi?

  1. Kuifanya biashara kutambulika kisheria
  2. Kutambulika na taasisi za fedha mfano benki (wakati wa kufungua akaunti).
  3. Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
  4. Kuongeza wigo wa kupata kazi na zabuni mbalimbali.
  5. Kuaminika kwa wateja

Vigezo kwa ajili ya kuomba leseni

(a) Mtu binafsi

  1. Namba ya kitambulisho cha taifa ya mwombaji wa leseni
  2. Namba ya utambulisho wa mlipakodi (TIN)
  3. Uthibitisho wa sehemu ya kufanyia biashara Mfano mkataba wa pango, leseni ya makazi au hati.
  4. Hati ya kuonyesha kutodaiwa kodi (Tax Clearance Certificate)
  5. Kibali kutoka mamlaka ya udhibiti (Kutegemea na aina ya biashara)

(b) Jina la biashara / kampuni

  1. Hati ya usajili wa kampuni au Jina la biashara
  2. Taarifa kutoka kwa msajili (extract from Register) kwa majina ya biashara pekee
  3. Namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) ya kampuni au mwenye jina la biashara.
  4. Hati ya kuonyesha kutodaiwa kodi (Tax Clearance Certificate) kwa anayehuisha leseni.
  5. Uthibitisho wa sehemu ya kufanyia biashara mfano mkataba wa pango, leseni ya makazi au hati ya kumiliki ardhi.
  6. Uthibitisho wa uraia na ukaazi kwa Wakurugenzi na Wanahisa wa kampuni.

Hatua 10 za kuomba  Leseni

  1. Tembelea www.business.go.tz
  2. Bofya sehemu iliyoandikwa "huduma"
  3. Chagua "huduma za Leseni"
  4. Bofya hatua ya kwanza "jisajili"
  5. Rejea kubofya sehemu iliyoandikwa "huduma"
  6. Chagua "huduma za Leseni"
  7. Hatua ya pili jaza taarifa za ombi la leseni
  8. Pakia viambatisho katika mfumo
  9. Bofya tuma ombi
  10. Thibitisha malipo.

ZINGATIA: Baada ya kutuma ombi, BRELA itapitia taaarifa zilizowasilishwa kama zipo sahihi kisha ankara ya malipo itatumwa kwa ajili ya kulipa na kuthibitisha malipo.