Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Lango la Mafanikio ya Biashara

Habari

TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 66 WA NCHIWANACHAMA WA SHIRIKA LA MILIKI UBUNIFU DUNIANI (WIPO)


TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO MKUU WA 66 WA NCHIWANACHAMA WA SHIRIKA LA MILIKI UBUNIFU DUNIANI (WIPO)

Tanzania inashiriki katika Mkutano Mkuu wa 66 wa NchiWanachama wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (World Intellectual Property Organization - WIPO) unaoendeleajijini Geneva, Uswisi, kuanzia tarehe 8 hadi 17 Julai2025.

Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na AfisaMtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara naLeseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa, na unajumuishapia Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Mashirika yaUmoja wa Mataifa Geneva, Dkt. Abdallah S. Possi, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani, Bi. Khadija Ngasongwa, pamoja na Mkurugenzi wa MilikiUbunifu kutoka BRELA, Bi. Loy Mhando.

Katika mkutano huo, Tanzania inasukuma mbele ajendaya ubunifu jumuishi, ikiwa na lengo la kuwawezeshavijana, wanawake na watu wenye mahitaji maalumkunufaika na kazi zao za ubunifu. Kupitia mikutano yaana kwa ana na viongozi wa WIPO, ujumbe waTanzania unalenga kuweka mikakati ya ushirikiano kwaajili ya kuandaa programu maalum za elimu nauhamasishaji kwa wadau mbalimbali, hususanwajasiriamali na wabunifu walioko katika maeneo yapembezoni.

Ushiriki wa Tanzania katika mkutano huu ni sehemu yajitihada za kukuza uchumi wa ubunifu na kuhakikishakuwa miliki bunifu inatambulika kama kichocheo cha maendeleo endelevu. Kupitia ushirikiano na WIPO, Tanzania inalenga kuwajengea uwezo wabunifuchipukizi katika kulinda na kuendeleza kazi zao, pamojana kuzigeuza kuwa bidhaa zenye thamani sokoni. Hililinaenda sambamba na juhudi za kuhakikisha usawa wafursa katika sekta ya ubunifu kwa makundi yote ya jamii.

Mkutano huu mkubwa unajumuisha nchi 193 wanachama wa WIPO na unatarajiwa kupitisha Mpangona Bajeti ya shirika hilo kwa mwaka wa fedha2026/2027. Kwa Tanzania, huu ni muda muafaka wakushiriki katika maamuzi ya kimataifa yanayohusu ulinziwa miliki bunifu na kuhakikisha kuwa mahitaji ya nchizinazoendelea yanazingatiwa katika sera na mikakati yakimataifa ya ubunifu.