Afisa Usajili kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bi. Fatma Jumanne akiwasilisha mada kwenye Semina ya urasimishaji biashara iliyoandaliwa na Taasisi ya Women Supporting Women, hivi karibuni kwa lengo la kuwapa mafunzo wajasiriamali wa taasisi hiyo, kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA ambazo ni Usajili wa Kampuni, Jina la Bishara, Alama za Biashara na Huduma, Hataza, kupata Leseni ya Kiwanda na Leseni kundi A