Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Ada za Hataza

Malipo yote yanalipwe kwa Msajili wa Kampuni ambapo watapewa stakabadhi. Waombaji wanaaswa kuepuka kufanya malipo pasi na kupewa stakabadhi za malipo. Matakwa ya malipo yoyote kwa afisa yeyote nje ya malipo yaliyobainishwa, yanapaswa kuripotiwa kwa simu zifuatazo: 2180113,2181344, 2180141 kwa hatua zaidi.

1. Uteuzi wa uwakilishi (mamlaka ya kisheria) sheria ndogo ya 7 (3) Hakuna ada
2. Maombi ya kupatiwa hataza (kifungu cha 2; sheria ndogo ya 8) SHT 12,000 /=
3. Maombi ya kupatiwa cheti cha utumizi (Vifungu 23 na 72) SHT 10,000 /=
4. Maombi ya cheti kutoka kwa Msajili kinachoidhinisha utolewaji wa sampuli kutoka katika mkusanyiko wa kitalu cha uoteshaji wa vimelea (sheria ndogo ya 10(2) SHT. 4,000 /=
5. Maombi ya Msajili ya kutaka taarifa kuhusu maombi ya nje, hataza au hati ya ulinzi (Sheria ndogo ya 20(1) Hakuna ada
6. Mwaliko wa kusahihisha  maombi kwa ajili ya kupewa cheti cha hataza au utumizi (Sheria ndogo ya 25 (1), 52) Hakuna ada
7. Taarifa ya uamuzi wa kupinga maombi ya kupewa cheti cha hataza au utumizi kwa sababu kutokidhi masharti rasmi (Sheria ndogo ya 25(2).52) Hakuna ada
8. Taarifa kuwa maombi ya kupewa cheti cha hataza au utumizi kinakidhi masharti rasmi (Sheria ndogo ya 25(3),52) Hakuna ada
9. Taarifa ya kutokidhi masharti thabiti na mwaliko wa kuwasilisha maombi ya uchunguzi na/au kubadili kwa ajili ya kupatiwa hataza (Sheria ndogo ya 26(3) Hakuna ada
10. Taarifa ya kupinga kutoa hataza kwa sababu ya kutokukidhi masharti (Kifungu cha 26(4) Hakuna ada
11. Taarifa ya uamuzi wa kutoa cheti cha hataza au utumizi (Sheria ndogo ya 28(1)(a)52) Hakuna ada
12. Kubadili maombi (Kifungu na. 20, sheria ndogo ya 22) SHT 8,000 /=
13. Kufungua jalada la marekebisho (Kifungu na. 25(3)(b); sheria ndogo na. 25 SHT 8,000 /=
14. Kufanya utafutaji wa ngazi ya kimataifa (Kifungu na. 26(2)(a): Sheria ndogo na. 26(1) SHT 10,000 /=
15. Kupatiwa hataza, Kifungu na. 28 sheria ndogo na. 28(1)(a) SHT 10,000 /=
16. Kutoa cheti cha utumizi (Vifungu na. 28 na 72 Sheria ndogo na. 27(1)(…na 52(1)) SHT 8,000 /=
17. Cheti cha kupewa hataza (Sheria ndogo na. 29(3) Hakuna ada
18. Cheti cha kupewa cheti cha utumizi (Sheria ndogo na. 29(3),52(1)(c) Hakuna ada
19. Ada ya mwaka kwa hataza (section 39(1); sheria ndogo 30
- Kumbukumbu ya mwaka wa kwanza SHT 4,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 2 SHT 5,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 3 SHT 6,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 4 SHT 7,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa SHT 8,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 6 SHT. 9,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 7 SHT. 10,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 8 SHT 11,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 9 SHT 12,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 10 SHT 13,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 11 SHT 14,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 12 SHT 15,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 13 SHT 16,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 14 SHT 17,000 /=
20. Ada ya mwaka kwa cheti cha utumizi (Vifungu na. 39(1) na 72(1): (Sheria ndozo na. 30 na 52))
- Maadhimisho ya mwaka wa 1 SHT 3,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 2 SHT 4,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 3 SHT 5,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 4 SHT 6,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 5 SHT 7,000 /=
- Maadhimisho ya mwaka wa 6 SHT 8,000 /=
21. Malipo ya ziada ya nyongeza ya muda wa malipo ya ada ya mwaka (Kifungu na 39 (2); Sheria ndogo na. 30 (3))
- Yasiyozidi mwezi mmoja SHT 1,000 /=
- Yasiyozidi miezi miwili SHT 2,000 /=
- Yasiyozidi miezi mitatu SHT 3,000 /=
- Yasiyozidi miezi minne SHT 4,000 /=
- Yasiyozidi miezi mitano SHT 5,000 /=
- Yasiyozidi miezi sita SHT 6,000 /=
22. Maombi ya kuongeza muda wa hataza (Kifungu na. 38(2); Sheria ndogo na. 31) SHT 12,000 /=
23. Maombi ya kurejesha cheti cha hataza au cheti cha utumizi ambacho muda wake umeisha au ya maombi ambayo yanaonekana yameondolewa (Sheria ndogo za 32.52) Hakuna ada
24. Kurejesha cheti cha hataza au utumizi ambacho muda wake umeisha au maombi ambayo yanaonekana yameondolewa (Sheria ndogo za 32.52) SHT 10,000 /=
25. Ofa ya kuachia cheti cha hataza au utumizi au dai (madai) yaliyomo katika cheti (Vifungu na. 62 na 72; Sheria ndogo 33(1) na 52) SHT. 8,000 /=
26. Taarifa ya pingamizi la ofa ya kuachia cheti cha hataza au utumizi au dai (madai) yaliyomo katika cheti (Sheria ndogo na. 33(2) na 52) SHT 10,000 /=
27. Maombi ya kufanya marekebisho ya jina, uraia, anwani au anwani ya huduma (Sheria ndogo 35) SHT 4,000 /=
28. Maombi ya kuandika mabadiliko ya umiliki, ya cheti cha hataza au utumizi au maombi kwa ajili ya kupata cheti cha hataza au utumizi (Sheria ndogo 36 na 52) SHT 4,000 /=
29. Maombi ya kufanya uchunguzi wa rejesta (Sheria ndogo 37(2) SHT 1,000 /=
30. Maombi ya nakala zilizopewa ithibati au sehemu ya nakala ya rejesta (Sheria ndogo 38) SHS 4,000 /=
31. Maombi ya kusahihisha dosari ndogo katika rejesta au katika waraka wowote ulioambatishwa (Sheria ndogo na. 39(1) SHT 1,500 /=
32. Maombi ya kusahihisha dosari ndogo zinazohusiana na hataza, maombi ya hataza, cheti cha utumizi au cheti cha maombi (Sheria ndogo 39(2) SHT 1,500 /=
33. Taarifa ya kusahihisha dosari ndogo zinazohusiana na cheti cha hataza au utumizi (Sheria ndogo 39(2) SHT 4,000 /=
34. Maombi ya kuandika kumbukumbu ya agizo au mahakama (Sheria ndogo 40) SHT 1,000 /=
35. Ombi la kusajili mkataba wa leseni (Kifungu cha 47; sheria ndogo 43) SHT 8,000 /=
36. Cheti cha kupokea ombi la usajili wa mkataba wa leseni  (sheria ndogo 44(1) Hakuna ada
37. Ombi la ingizo katika rejesta kwa ujumla leseni chini ya vyeti vya hataza au utumizi vinapatikana kama haki kama inavyoelezwa katika (Kifungu 60(1) na 72, sheria ndogo 5091) na 52) Hakuna ada
38. Cheti cha usajili wa mkataba wa leseni (sheria ndogo 46) Hakuna ada
39. Ombi la kubadilisha maombi kwa ajili ya cheti cha utumizi kuwa maombi ya hataza au kinyume chake (kifungu 74; sheria ndogo 52(2) SHT 5,000 /=
40. Ombi la kubadilisha maombi ya hataza kuwa maombi ya cheti cha utumizi (kifungu 74; sheria ndogo 52(2) SHT 3,000 /=
41. Pingamizi la polisi katika ombi la ingizo linatekelezwa kwa sheria ndogo ya 50(1) (Kifungu 60(3) sheria ndogo 50(2) TSHS 10,000 /=
42.  Maombi ya kufuta ingizo yanatekelezwa chini ya sheria ndogo 50(1) (Kifungu 60(7) TSHS 1,500 /=
43. Maombi ya kuongeza muda wa mwisho (Sheria ndogo 55(1) Hakuna ada
44. Kutoa nakala za nyaraka chini ya kifungu 5(c) kwa ukurasa TSHS 300 /=
45. Ombi la On request for bearing (regulation 65) TSHS 10,000 /=
46. Ada ya uhamishaji kwa ajili ya maombi ya kimataifa (Kifungu 53) SHT 5,000 /=
47. Ada kwa ajili ya maandalizi nakala za maombi ya kimataifa kwa ukurasa 53 TSHS 1,500 /=
48. Ada maalum inayorejelea Kifungu 32(1)(b) na (2)(b) SHT 4,000 /=