Huduma Zetu
UTOAJI WA LESENI ZA VIWANDA
Kiwanda ni nini?
Ni shughuli inayohusisha uzalishaji kwa kubadilisha malighafi kuwa bidhaa au
muundo wa kitu kinachofaa kwa matumizi.
Aina za Viwanda
- Viwanda vidogo – hivi huwa na kiasi cha uwekezaji kisichozidi Sh.100,000,000/-
- Viwanda vikubwa – hivi huwa na kiasi cha uwekezaji kinachozidi Sh. 100,000,000/-
Faida za kusajili/kuwa na leseni ya kiwanda ni zipi?
- Kutambulika na taasisi za fedha kama vile benki (wakati wa kufungua akaunti).
- Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
- Kuongeza wigo wa kupata kazi na zabuni mbalimbali.
Nyaraka za kuambatisha
- Mchanganuo wa mradi
- Uthibitisho wa mahali kilipo kiwanda
- Fomu ya majumuisho (consolidated form)
Hatua 10 za kusajili kiwanda
- Tembelea www.brela.go.tz au ors.brela.go.tz
- Ingia katika akaunti yako ya usajili kwa njia ya mtandao (ORS) au tengeneza akaunti katika mfumo.
- Chagua huduma mtandao.
- Chagua leseni ya kiwanda.
- Chagua aina ya huduma.
- Jaza kiasi cha uwekezaji.
- Jaza taarifa za kiwanda husika.
- Pakia viambatisho katika mfumo.
- Lipa kwa njia ya simu au benki.
- Maombi yatafanyiwa kazi baada ya malipo kupokewa.