Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Huduma Zetu

USAJILI WA KAMPUNI

Kampuni ni nini?

Kampuni ni mjumuiko wa watu wawili au zaidi wenye nia ya kufanya biashara halali na kuusajili mjumuiko huo chini ya Sheria ya kampuni.

Aina za Kampuni

 1. Kampuni ya kigeni
 2. Kampuni binafsi
 3. Kampuni ya umma

Faida za Urasimishaji Kampuni ni zipi?

 1. Kuipatia utu wa kisheria biashara yako
 2. Kutambulika na taasisi za fedha mf. benki wakati wa kufungua akaunti.
 3. Kupata mikopo katika taasisi za fedha kama benki.
 4. Kupanua wigo wa kufanya biashara kubwa, mf. biashara za kimataifa
 5. Urahisi wa kuitangaza kampuni kwa urahisi na kupanua wigo wa wateja.

Vigezo vya kusajili Kampuni

 1. Mwombaji anatakiwa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA
 2. Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA ya kila mwanahisa
 3. Namba ya kitambulisho cha Taifa kutoka NIDA au pasi ya kusafiria kwa raia wa kigeni na namba ya utambulisho wa mlipakodi (TINya kila mkurugenzi

Nyaraka za kuambatisha

 1. Katiba ya Kampuni
 2. Fomu ya uadilifu
 3. Fomu ya majumuisho (Consolidated Form)

Hatua 10 za kusajili Kampuni

 1. Tembelea "www.brela.go.tz" au "ors.brela.go.tz".
 2. Ingia katika akaunti yako ya Usajili kwa njia ya mtandao (ORS) au tengeneza akaunti katika mfumo.
 3. Chagua "huduma mtandao".
 4. Chagua "kampuni".
 5. Chagua "aina ya huduma".
 6. Chagua "aina ya kampuni".
 7. Jaza taarifa za kampuni husika.
 8. Pakia viambatisho katika mfumo.
 9. Lipa kwa njia ya simu au benki.
 10. Maombi yatafanyiwa kazi baada ya malipo kupokewa.