Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Huduma Zetu

UTOAJI WA HATAZA

HATUA ZA USAJILI WA HATAZA KWA NJIA YA MTANDAO

 1. Mtumiaji ataingia kwenye tovuti ya BRELA www.brela.go.tz na kupata link ya usajili kwa njia ya mtandao
 2. Mwombaji akishaingia kwenye kurasa ya usajili kwa njia ya mtandao (https://ors.brela.go.tz/ors) analazimika kufungua akaunti ili aweze kutumia huduma za BRELA zitolewazo kwa njia ya mtandao. Ili kutengeneza akaunti kwa mtanzania analazimika kuwa na namba ya utambulisho wa utaifa na kwa wasio raia wa Tanzania namba ya pasi ya kusafiria pamoja na taarifa za barua pepe, namba ya simu ya mkononi na kutengeneza nywila (password)
 3. Baada ya kutengeneza akaunti mwombaji atatumiwa jina la kutumia kwenye akaunti yake pamoja na link “ku-activate” akaunti na kisha kuingia kwenye akaunti yake kwa ajili ya kupata huduma zinazotolewa.
 4. Mteja atakapoingia kwenye akaunti yake atachagua sehemu ya “huduma mtandao” (new e-service).
 5. Ndani ya huduma mtandao kuna huduma zote zitolewazo na BRELA ambazo ni Makampuni, Majina ya Biashara, Alama za Biashara na Huduma, Hataza, Leseni za Viwanda na Huduma za taarifa, mteja atachagua huduma anayohitaji Hataza.
 6. Mteja anapochagua Hataza mfumo utamuwezesha kuingiza taarifa za usajili mpya au maombi mengineyo yanayohusiana na Hataza.
 7. Mtumiaji wa mfumo atachagua huduma ya usajili wa Hataza.
 8. Mwombaji atachagua maombi mapya ya hataza.
 9. Ataingiza taarifa za uwakilishi (Representation Statement), hapa atasema mwombaji anaomba kama nani, mmiliki au mwakilishi.
 10. Mwombaji ataingiza maelezo ya kitaalam (Technical description)
 11. Atachagua aina ya maombi kama ni ya “PCT” (hataza ya kimataifa kupitia Shiriki la Miliki Ubunifu la Dunia) au aina nyingine (other) ambapo atachagua aina ya hataza.
 12. Atajaza kichwa cha habari cha uvumbuzi
 13. Ataweka maelezo ya utangulizi ya uvumbuzi
 14. Ataonyesha rejea ya namba ya mwisho ya ukurasa wa madai ya uvumbuzi (claims)
 15. Mwombaji ataweka rejea ya namba ya ukurasa wa mwisho wa maelezo ya hitimisho ya uvumbuzi (description)
 16. Ataweka maelezo ya dhahania ya uvumbuzi (Abstract)
 17. Atajaza taarifa za madai ya uvumbuzi (claims)
 18. Mwombaji atajaza taarifa za mmiliki wa Hataza
 19. Atajaza taarifa za mwakilishi (Agent) kama maombi yanawasilishwa na mwakilishi
 20. Mwombaji atajaza taarifa za Mvumbuzi (inventor)
 21. Mwombaji atajaza taarifa za maombi ya awali aliyowasilisha nchi nyingine ikiwa atataka tarehe itambulike hapa nchini kama ndio tarehe ya maombi (isizidi miezi 12 toka tarehe maombi yanawasilishwa katika nchi nyingine.
 22. Ataonyesha kama hataza inahusiana na hataza ambayo ilishawasilishwa kabla (Divisions)
 23. Baada ya kuingiza taarifa zote atabonyeza kitufe cha endelea “proceed”
 24. Mfumo utatengeneza fomu ambayo itakuwa na taarifa zote alizoingiza mteja “consolidated form” mteja atatakiwa kuidownload fomu, kuprint na kuweka sahihi zao na endapo mmiliki ni kampuni atatakiwa kugonga muhuri wake.
 25. Mfumo utampeleka kwenye dirisha la kuambatanisha viambatanishi ambayo ni ; fomu (consolidated form) kwenye muundo wa “PDF”, atatakiwa kuambatanisha nyaraka / taarifa ya hataza (patent document), mchoro wa hataza husika (kama ipo) ikiwa kwenye muundo wa “JPEG”,kama kuna na “priority claim” atatakiwa kuambatanisha “priority documents”, kama muombaji atakuwa ni muwakilishi atatakiwa kuambatanisha fomu Na. 1 ya uwakilishi.
 26. Baada ya hapo tabonyeza kitufe cha endelea na mfumo utampeleka kwenye malipo ambapo atachagua njia ya malipo atakayotumia (simu au benki)
 27. Mwombaji atachagua sehemu ya kukubali vigezo na masharti
 28. Baada ya malipo maombi yanatumwa BRELA na mteja anaweza kuprint risiti yake kwa kubonyeza kitufe cha “download receipt”
 29. BRELA watafanyia kazi maombi
 30. Baada yakukamilisha mteja anapokea ujumbe kwenye barua pepe na namba ya simu aliyoweka kwenye mfumo, ujumbe utamtaarifu matokeo ya ombi ambayo ajayaona sehemu ya maombi (applications) atafungua ombi husika na ataweza kuona matokeo hayo sehemu ya “print-outs”
 31. Kama ombi litakuwa na mapungufu atapokea ujumbe kwa barua pepe kumtaarifu kuhusu mapungufu ambapo kwenye ombi lake atapata maelekezo ya vitu vya kurekebisha kwa kufungua sehemu ya “my list” na kufungua ombi husika ili arekebishe. Akishafanyia marekebisho atatuma tena BRELA kwa ajili yakufanyiwa kazi.