Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Huduma Zetu

USAJILI WA ALAMA ZA BIASHARA NA HUDUMA

Alama ya biashara au huduma (Nembo) ni nini?

Ni alama ya kipekee inayotambulisha bidhaa au huduma fulani inayozalishwa au kutolewa na mtu au kikundi fulani. Alama hizi husaidia wafanyabiashara tofauti wanaozalisha bidhaa za aina moja kuzitofautisha bidhaa zao ziingiapo sokoni.

Faida za kusajili alama ya biashara au huduma (Nembo) ni zipi?

  1. Kumwezesha mbunifu wa alama kutambulisha na kutangaza bidhaa au huduma sokoni.
  2. Kuhimili ushindani katika soko.
  3. Kumpa haki ya kipekee ya kutumia alama husika.
  4. Kuwawezesha watumiaji wa bidhaa au huduma kuitambua na kuichagua kwa kuangalia alama.
  5. Kumpatia mbunifu wa alama husika kipato kwa  njia ya kuuza Alama au kutoa haki ya matumizi kwa mtu mwingine

Vigezo vya kusajili Alama ya biashara au huduma

  1.  Alama iwe ya kipekee ambayo ameibuni mmiliki mwenyewe.
  2.  Alama hiyo isifanane na alama ambayo ilishasajiliwa na mtu mwingine katika daraja husika.
  3. Isielezee sifa ya bidhaa au huduma inayohusu daraja husika.
  4. Isiwe kinyume cha sheria na maadili.

Nyaraka za kuambatanisha

  1. Picha au mchoro wa alama
  2. Fomu ya majumuisho (Consolidated form)
  3. Fomu TM/SM 1 kama mwombaji ni mwakilishi

Hatua za kusajili Alama ya biashara au huduma

  1. Tembelea www.brela.go.tz au ors.brela.go.tz
  2. Ingia katika akaunti yako ya Usajili kwa Njia ya Mtandao (ORS) au tengeneza akaunti katika mfumo.
  3. Chagua "huduma mtandao"
  4. Chagua "Alama ya biashara/huduma"
  5. Chagua aina ya huduma
  6. Jaza taarifa za Alama ya biashara au huduma husika
  7. Pakia viambatisho katika mfumo.
  8. Lipa kwa njia ya simu au benki.
  9. Maombi yatafanyiwa kazi baada ya malipo kupokewa.