Habari
BRELA MSHINDI WA TATU TUZO ZA TAASISI WEZESHI KWA BIASHARA NCHINI
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA leo tarehe 13 Julai, 2026 imetunukiwa tuzo ya kuwa Taasisi Bora kwa kuwezesha biashara kwenye Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam (Sabasaba).
BRELA imekabidhiwa tuzo hiyo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa kufunga maonesho hao ambayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni hadi tarehe 13 Julai 2026.
Kwa upande wake Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Seka Kasera ambaye pia ni Meneja kutoka Kurugenzi ya Miliki Ubunifu, sehemu ya Alama za Biashara na Huduma akizungumza baada kupokea tuzo hiyo alisema ushindi huo ni faraja kwa taasisi kwakuwa maboresho ya mfumo wa BRELA Online System (BOS) yamepokelewa vizuri na wadu wote.
“Sisi kama BRELA Maonesho haya ya 50 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam yalikuwa ya kipekee, tumeyachukulia kwa uzito mkubwa kama ilivyo kwa miaka yote kwa sababu ndipo tunapofahamu wateja wetu wanataka nini na sisi tunataka nini ili tuweze kwenda, tunafurahi wateja wametupokea vizuri” Alisema Bw. Kasera.
Aidha katika maonesho hayo, BRELA imefanikiwa kuwahudumia zaidi ya wafanyabiashara 1200 kutoka maeneo mbalimbali kwa kutoa huduma za sajili na leseni papo kwa hapo, elimu katika makundi maalum kama vile vijana na wanawake.
BRELA imepata tuzo hiyo baada ya kushika nafasi ya tatu kwenye kundi lililojumuisha taasisi wezeshi kwa biashara nchini Tanzania ambapo mshindi wa kwanza ni Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na mshindi wa pili akiwa ni Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
