Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA WATAMBUENI WABUNIFU WANUFAIKE NA KAZI ZAO


 

BRELA WATAMBUENI WABUNIFU WANUFAIKE NA KAZI ZAO

SERIKALI imeielekeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kuwatambua wabunifu na kuhakikisha wanapata dhamana zinazowawezesha kukopesheka Ili kunufaika na ubunifu wao.

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt.Ashatu Kijaji ametoa rai hiyo, katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Naibu Waziri wa Utamaduni ,Sanaa na Michezo Mhe.Hamisi Mwinjuma leo tarehe 9 Mei,2024 jijini Dar es Salaam katika maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu duniani.

"Wapo wabunifu wengi nchini ambao ubunifu wao hawajanufaika nao,hivyo Kwa kuwatambua itasaidia kupata mikopo kutoka benki mbalimbali ambayo wataitumia kujiendeleza na kunufaika zaidi na kutawezesha kutatua changamoto na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja nchini." amesema.

Amesema Kwa upande wa serikali itahakikisha kuweka mazingira na sera imara katika kuimarisha miliki bunifu nchini na kwamba maendeleo ya nchi yanategemea miliki bunifu kwa ukuaji wa uchumi.

Serikali ina uhakika kuwa miliki bunifu zitaondoa changamoto kwa jamii na zitaongeza ukuaji wa uchumi Kwa mtu mmoja mmoja,"amesema Mwinjuma.

Mwinyijumaa amesema anatambua kazi nzuri inayofanywa na BRELA katika kuwaimarisha wafanyabiashara na wenye makampuni kutekeleza shughuli zao za kimaendeleo na kwamba itahakikisha ifikapo mwaka 2030 kunakuwa na uwiano wa maendeleo duniani kwa kutumia miliki bunifu",amesema.

Aidha ameongeza kuwa, Serikali kwa kushirikiana na Taasisi nyingine itawezesha ukamilikaji wa sera ya miliki bunifu ambayo italeta mwanga katika kusimamia mwongozo wa hati miliki Tanzania.

Aidha aliitaka BRELA inapoazimisha maadhimisho hayo yatumike kama fursa ya kujadili na yatolewe maoni yatakayofanyiwa kazi.

Naye, Ofisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa amesema masuala ya ubunifu yatasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo mbele na kwa hivi Sasa taasisi inampango wa kuanzisha programu ya miliki bunifu katika vyuo vyote nchini lengo ni kuendeleza ubunifu nchini.

Nyaisa amesema nchi nyingi zinaendelea duniani kwa sababu ya kueneza miliki bunifu sehemu mbalimbali ndani ya nchi zao.

Naye Mwenyekiti wa bodi ya ushauri BRELA Profesa Neema Mori amesema Maadhimisho hayo ni muhimu kuendelea kusheherekewa nchini kwani yanatoa fursa ya kukutanisha wadau mbalimbali na kuweza kujadiliana,kujifunza na kupata fursa ambazo zitasaidia kukuza bunifu za wabunifu nchini.

Amesema kufuatia maboresho yanayofanywa ndani ya BRELA yanasababisha kupokea wageni wengi kuja kujifunza wakiwemo Burundi pamoja na Sudani Kusini.
Mwishooo