Habari
BRELA YATOA MAFUNZO MAALUMU CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM
BRELA YATOA MAFUNZO MAALUMU CHUO CHA TAALUMA YA POLISI DAR ES SALAAM
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewashauri wanafunzi wa kozi za Uafisa na Ukaguzi Msaidizi kutoka Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam kujiandaa na maisha baada ya Utumishi wa Umma kwa kuanzisha na kuwekeza kwenye biashara mbalimbali zilizorasimishwa ili kuepuka changamoto wanazopata baada ya kustaafu.
Ushauri huo umetolewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Bw. Godfrey Nyaisa wakati wa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo Maafisa 780 na Wakaguzi Wasaidizi 175 katika chuo hicho kufahamu kazi mbalimbali zinazofanywa na BRELA pamoja na maeneo ambayo taasisi hizo mbili za Serikali zinavyoshirikiana katika kubadilishana taarifa.
“Tuko hapa kwaajili ya kupeana uelewa, mimi niwashauri wale ambao hawajaanza biashara ni hatari sana kuanza biashara baada ya kustaafu ni hatari mmono, mtu anaweza kukuambia biashara ya malori inalipa, wewe unastaafu unaingia kwenye hiyo biashara unanunua lori unamkabidhi dereva na siku dreva anaweza akakuudhi matokea yake unapata shinikizo la damu” alisema Bw. Nyaisa
Aidha, Bw. Nyaisa amewataka pia maafisa hao kuzitumia kwa uadilifu na uaminifu taarifa mbalimbali wanazoziomba kutoka BRELA katika misingi ya kazi na si vinginevyo na kuepuka kusambaa kwa taarifa hizo kwa watu embat sio waaminifu na waadilifu katika kazi.
“BRELA inapokea barua tano hdi kumi kwa siku zikiomba taarifa za makampuni au watu mbalimbali, zile taarifa tunazowapa mzitumie katika misingi ya kazi ambayo mmeziombea na si vinginevyo, kwa sasa tumeamua kutakuwa na kituo kimoja kupitia ofisi ya DCI na yeye ndiye atakuwa anatoa taarifa hizo. Mfano kwa Dar es Salaam vituo vyote vitakuwa vinaomba taarifa kwenye kituo hicho kwa sabbat mfumo wetu tayari umewapa ruhusa” Alisisitiza Bw. Nyaisa
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Dkt. Lazaro Mambosasa, amesema mafunzo hayo yaliyotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ni muhimu na yatawasaidia maofisa hao katika kazi zoo na maista yao baada ya utumishi wa umma.
Mafunzo waliyopewa wanafunzi wa kozi za Uafisa na Ukaguzi Msaidizi kutoka Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam yalijikita zaidi kwenye shughuli za BRELA kama vile Usajili wa Kampuni, Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za Biashara na Huduma Utoaji wa Leseni za Biashara kundi A pamoja na Utoaji wa Hataza