Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

BRELA YAWAFIKIA WANAFUNZI ZAIDI 2000 JIJINI MWANZA


 

BRELA YAWAFIKIA WANAFUNZI ZAIDI 2000 JIJINI MWANZA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imewafikiwa wahadhiri pamoja na wanafunzi zaidi ya 2,000 katika zoezi la kutoa elimu ya Miliki Ubunifu katika Vyuo Vikuu na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), jijini Mwanza.

Elimu hiyo iliyoanza kutolewa tarehe 8 Mei, 2023 imehitimishwa leo tarehe 12 Mei, 2023 katika chuo.cha VETA.

Katika mafunzo hayo Wahadhiri pamoja na Wanafunzi wameelekezwa kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA, upande wa Alama za Biashara na Huduma pamoja na Hataza

Akielezea huduma zinazotolewa na BRELA kwa Wahadhiri pamoja na Wanafunzi wa Chuo VETA , Afisa Mwandamizi kutoka BRELA, Bw. Raphael Mtalima amewataka Wahadhiri hao wanapowafundisha wanafunzi wasisite kuwakumbusha kuwa watakaporasimisha biashara zao itawafungulia wigo wa kutambulika na mamlaka mbalimbali na pia kuwawezesha kukopesheka katika Taasisi za kifedha.

BRELA inaendelea na kampeni ya kutoa elimu katika Vyuo mbalimbali nchini ili kukuza uelewa wa masuala ya Miliki Ubunifu pamoja na huduma zote zinazotolewa na Wakala.

Kampeni hii ya kutoa elimu kwa Wanafunzi vyuoni ni endelevu ambayo ilianza rasmi Mkoani Mbeya na kufuatiwa na mkoa wa Mwanza na itaendelea katika mikoa mingine nchini, lengo kuu ni kuhakikisha elimu hii inawafikia Wanafunzi wengi zaidi waliopo vyuoni.

Mafunzo ya Miliki Ubunifu Jijini Mwanza, yamefanyika katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Mwambata-Bugando, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo ( SIDO), pamoja na Chuo cha VETA.