Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

MKURUGENZI MANISPAA YA TEMEKE ARIDHISHWA NAMNA BRELA INAVYOTOA MAFUNZO KWA JAMII


MKURUGENZI MANISPAA YA TEMEKE ARIDHISHWA NAMNA BRELA INAVYOTOA MAFUNZO KWA JAMII.

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imepogezwa kutokana na jitihada inazozifanya za kutoa elimu na mafunzo kwa jamii ili kukuza uelewa wa wananchi inaowahudumia.

Pongezi hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Temeke Bw. Elihuruma Mabelya, alipotembelea banda la BRELA tarehe 23 Mei, 2023 katika "Tamasha la kijana Janjaruka na Fursa". Iinaofanyika katika viwanja vya Zakhiem- Mbagala, Jijini Dar es Salaam.

Akiwa katika banda la BRELA Mkurugenzi huyo ameshuhudia muitikio wa wananchi wa Temeke katika kupata elimu na huduma za papo kwa papo zinazotolewa na Taasisi katika tamasha hilo.

Awali Mkurugenzi huyo alielezwa na Afisa Usajili Mwandamizi wa BRELA Bw. Nassoro Mtavu namna BRELA inavyoshiriki kutoa elimu kwa umma mbali ya kushiriki kwenye matamasha na maonesho mbalimbali, kuwa ni pamoja na kutembelea taasisi za elimu ya juu na ya kati, kushiriki katika semina na makongamano pamoja na kutoa elimu kwa njia ya redio, televisheni na mitandao ya kijamii.

Bw. Mtavu amewasihi wananchi wa Temeke kutumia fursa iliyopo kwa kufika katika banda la BRELA ili kupata huduma na kutatuliwa changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wakati wa usajili katika mfumo wa Usajili kwa njia ya Mtandao.