Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Tunaipa Uhai wa Kisheria Biashara yako

Habari

SHERIA NA KANUNI NDIO NGUZO ZA UTOAJI WA HUDUMA ZA BRELA


SHERIA NA KANUNI NDIO NGUZO ZA UTOAJI WA HUDUMA ZA BRELA

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imebainisha kwamba katika utekelezaji wa wa majukumu yake nguzo zake kuu ni sheria sita ambazo inazisimamia pamoja na kanuni zake.

Hayo yamebainishwa Januari 24, 2023 jijini Dodoma kwenye Viwanja vya Nyerere Square na Afisa Leseni wa BRELA Bi. Winfrida Gaudence, wakati Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma alipotembelea banda la BRELA katika Wiki ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria nchini.

Bi. Gaudence ameeleza kuwa Wakala ilianzishwa chini ya Sheria ya Wakala za Serikali Sura Na. 245 na inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria 6.
Majukumu hayo ni Kusajili Kampuni (The Companies Act, Cap. 212);
Kusajili Majina ya Biashara (The Business Names (Registration) Act, Cap. 213 R.E. 2002);
Kusajili Alama za Biashara na Huduma (The Trade and Service Marks Act, Cap. 326 R.E. 2002);

Kutoa Hataza (The Patents (Registration) Act, Cap. 217 R.E. 2002);
Kutoa Leseni za Viwanda (The National Industries (Licensing and Registration) Act, Cap 46 R.E. 2002);

Kutoa Leseni za Biashara Kundi "A" (The Business Licensing Act Cap. 208 R.E. 2002).

Ameeleza kuwa katika maonesho hayo BRELA itatoa huduma kwa siku kumi (10) mfululizo ambapo huduma hizo zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 23 Januari, 2023 na hitimisho litakuwa tarehe 1 Februari, 2023.

Naye Msimamizi wa Ofisi ya Kanda ya Kati iliyopo Dodoma, Bw. Gabriel Girangay ametoa wito kwa wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kufika katika madhimisho hayo ili kupata ufafanuzi wa kisheria.

“Kwanza kabisa kwa mteja yeyote anayefika hapa tunamhudumia na kumaliza changamoto yake hapa hapa, kipaumbele chetu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu hawaondoki na changamoto zao kurudi nyumbani”, amesema Bw. Girangay.

Maadhimisho ya Wiki ya Sheria kwa mwaka 2023 yanafanyika Kitaifa Jijini Dodoma na yalizinduliwa Rasmi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, yakiwa na kauli mbiu “Umuhimu wa Utatuzi wa Migogoro kwa njia ya Usuluhishi katika Kukuza Uchumi Endelevu; Wajibu wa Mahakama na Wadau".