Karibu katika tovuti hii ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA). Katika tovuti hii utapata taarifa kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA, nj... Soma zaidi
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Mhe. Balozi Waziri Rajab Salum akitoa salamu wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wizara na Maafisa Biashara Nchini, kilichofanyika tarehe 17 Agosti 2026, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo akifungua Kikao Kazi cha Wizara na Maafisa Biashara Nchini, kilichofanyika tarehe 17 Agosti 2026, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dennis Londo (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Wizara na Maafisa Biashara Nchini, kilichofanyika tarehe 17 Agosti 2026, katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipokea gawio la BRELA kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA Prof. Neema Mori (Kushoto). Kulia kwake ni Bw. Godfrey Nyaisa, Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA.
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imetoa mafunzo kwa Majaji wa Mahakama Kuu na Manaibu Wasajili wa Divisheni ya Biashara kuhusu haki za miliki ubunifu kwa lengo la kuimarisha usimamizi na ulinzi wa haki hizo nchini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Salvio Kapinga (wa nne kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa michezo waliotunukiwa tuzo wakati wa maadhimisho ya siku ya Miliki Ubunifu Duniani iliyofanyika tarehe 08 Mei, 2026 katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam.
MAADHIMISHO YA SIKU YA MILIKI UBUNIFU DUNIANI
Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu BRELA Bi. Loy Mhando (wa nne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau wa michezo baada ya warsha ya elimu kuhusu Miliki Ubunifu na Michezo iliyofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 05 Mei, 2026. Anayefuatia kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mhandisi Leodigar Tenga.
Watumishi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye sherehe za maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kitaifa Mei Mosi imefanyika mkoani Njombe.
Mfumo wa BOS
Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA, Profesa Neema Mori (Kulia) akikabidhi baadhi ya mahitaji kwa Bw. Hamis Suleiman mlezi wa Kituo cha New Faraja Orphanage, Mburahati Dar es Salaam. Kulia ni Bi. Yvonne Massele Afisa Usajili kutoka Kurugenzi ya Miliki Ubunifu BRELA.
Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu BRELA, Bi. Loy Mhando (aliyeketi Katikati) aakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wanafunzi wa Klabu ya Miliki Ubunifu Chuo Kikuu cha Mzumbe Ndaki ya Mbeya, walezi wao na baadhi ya watumishi wa BRELA kutoka Kurugenzi ya Miliki Ubunifu.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (aliyeketi katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Menejimenti ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) baada ya kuzindua kikao cha pili cha Baraza la Wafanyakazi wa BRELA kwa mwaka wa fedha 2025/2026 kilichofanyika jijini Mwanza Machi 04, 2026.