Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni

Lango la Mafanikio ya Biashara

Habari

BRELA YATUNUKIWA CHETI CHA HESHIMA, HAFLA YA INCLUSIVE MWALIMU GALA 2026


Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) tarehe 02 Agosti 2026, ulitunukiwa Cheti cha Heshima kufuatia ushiriki wake katika warsha ya Inclusive Mwalimu Gala 2026 iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

BRELA imekabidhiwa cheti hicho na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ambaye alipongeza jitihada za taasisi mbalimbali zinazounga mkono sekta ya elimu nchini ikiwemo BRELA.

Katika warsha hiyo iliyowakutanisha walimu, wahadhiri vyuo vya elimu ya juu na kati, wanawake wataalam, wajasiriamali, wanafunzi na wadau mbalimbali wa maendeleo, BRELA ilitumia fursa ya ushiriki wake kwa kutoa mafunzo juu ya faida za kufanya biashara kupitia mifumo rasmi ya kisheria.

Akizungumza wakati wa kuwasilisha, Afisa Usajili wa BRELA Bw. Benedickson Wilson alibainisha kuwa urasimishaji wa biashara kupitia huduma za usajili wa makampuni, majina ya biashara, Alama za Biashara na Huduma, Leseni za Biashara Kundi A na Leseni za Viwanda ni nguzo muhimu inayomlinda mjasiriamali.

"Urasimishaji sio tu suala la kisheria, bali ni ngao ya kiuchumi, unaposajili kampuni yako na kupata leseni, unalinda jina la biashara yako lisitumike na mtu mwingine na unajenga uaminifu mkubwa mbele ya wateja na washirika wa kibiashara," alibainisha Bw. Wilson. 

Tuzo hii ya heshima inaashiria nafasi muhimu inayoshikiliwa na BRELA si tu kama msajili, bali kama mdau mkubwa anayechochea maendeleo jumuishi kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mifumo ya kisasa na ya kidijitali