Habari
HUDUMA YA USAJILI WA HAKI YA DHAMANA INAYOWEKWA JUU YA MALI ZA KAMPUNI
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), inapenda kuzitaarifu Kampuni,Taasisi za Kifedha, Ofisi za Wanasheria na wadau wote kuwa huduma za uwasilishaji wa usajili wa haki ya dhamana kwenye mali za kampuni (Charges) sasa zinafanyika kupitia mfumo ulioboreshwa wa BRELA Online Service (BOS).
Awali huduma hii ilikuwa inamuhitaji mteja kufika katika ofisi za BRELA, ila kwa sasa wanaweza kuwasilisha nyaraka zote za haki ya dhamana kwenye mali za kampuni (Charges) kwa njia ya mtandao. Maboresho hayo yamelenga kurahisisha utoaji wa huduma kwa haraka na ufanisi zaidi.
Ili kuwasilisha maombi hayo mwombaji atapaswa kuanza kufungua akaunti itakayomwezesha kupata huduma tajwa na hatua ya pili ni kuchagua huduma za kampuni (Company Services) na kuelekea kwenye kipengele cha huduma za dhamana (Charges Services). Katika sehemu hiyo, atakuta usajili wa dhamana hizo (Registration of Charges). Baada ya hapo, mteja atatakiwa kwenda kwenye kitufe cha kusajili dhamana mpya (Register New Charges), kisha kujaza namba ya usajili wa kampuni husika na kuendelea na hatua zinazofuata sambamba na kujaza Fomu Namba 99 inayopatikana kwenye tovuti ya www.brela.go.tz
Kwa wateja ambao bado hawajafungua akaunti katika mfumo wa BOS, wanatakiwa kutengeneza akaunti zao kwa kutembelea tovuti rasmi ya https://bos.brela.go.tz na kubonyeza kitufe kilichoandikwa "Create New Account". Baada ya kujaza taarifa zinazohitajika, mtumiaji atapokea ujumbe mfupi na maelekezo kupitia barua pepe yake (email) yatakayomwezesha kuingia rasmi na kuanza kutumia mfumo huo wa kidijitali kwa ajili ya maombi yake.
Kwa usaidizi wa haraka, tafadhali wasiliana nasi kupitia namba ya simu +255 (0) 22 2212800 au andika kupitia barua pepe support.bos@brela.go.tz
