Habari
HUDUMA YA UTOAJI WA LESENI ZA BIASHARA KUNDI “A”
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inapenda kuwataarifu wadau wote na umma kwa ujumla kuwa huduma zote za utoaji wa Leseni za Biashara Kundi “A”, ambazo awali zilikuwa zinapatikana kupitia mfumo wa Tanzania National Business Portal (TNBP), sasa zinapatikana kupitia mfumo wa BRELA Online Services (BOS).
Kutokana na mabadiliko hayo, mteja ambaye ni mmiliki wa Kampuni au Jina la Biashara na alikuwa na Leseni ya Biashara katika mfumo wa TNBP anatakiwa kufungua akaunti katika mfumo wa BOS kwa kutumia barua pepe ((Email) ) ya mwanahisa, mkurugenzi au katibu wa kampuni inayotumika katika mfumo wa Online Registration System (ORS) pamoja na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa Mtanzania au Hati ya Kusafiria (Passport) kwa raia wa kigeni.
Vilevile kwa mmiliki wa jina la biashara atatumia barua pepe (Email) anayotumia kwenye mfumo wa Online Registration System (ORS) pamoja na Namba ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kwa Mtanzania au Hati ya Kusafiria (Passport) kwa raia wa kigeni.
Aidha, kwa upande wa mtu binafsi aliyekuwa na Leseni ya Biashara katika mfumo wa TNBP anatakiwa kufungua akaunti katika mfumo wa BOS kwa kutumia barua pepe ((Email) ) ileile aliyotumia wakati wa usajili wa akaunti yake katika mfumo wa TNBP.
Kwa maelezo zaidi au usaidizi wa haraka, tafadhali wasiliana nasi kupitia simu +255 (0) 22 2212800 au tutumie barua pepe kupitia support.bos@brela.go.tz.
